MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

CHARITY EVENT Mafunzo

Posted by admin on 2025-06-13 13:30:53 | Last Updated by admin on 2025-09-19 10:50:05

Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 94


MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

Equip for Change yaadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa Semina ya Uhamasishaji Kata ya Miono, Wilaya ya Bagamoyo.

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika 2025, Equip for Change iliendesha semina maalum ya uhamasishaji juu ya haki, ulinzi na usalama wa mtoto katika Kijiji cha Miono, Kata ya Miono, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.


Semina hii iliyofanyika tarehe 12 Juni 2025, iliwaleta pamoja wanawake 70 na watoto 30 kutoka shule za msingi na sekondari kwa lengo la kujadili kwa kina masuala yanayohusu haki za binadamu, haki za mtoto, pamoja na aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia unaowaathiri watoto na wanawake katika jamii ya watu wa Miono.


Washiriki walipata maarifa juu ya vyanzo vya ukatili, madhara yake, mbinu za kujilinda, na hatua za kuchukua katika kutoa taarifa na kuripoti matukio ya ukatili. Kwa njia ya mijadala, masimulizi na mafundisho, semina ilichochea mjadala wa kina kuhusu wajibu wa jamii nzima katika kulinda watoto na kuendeleza malezi chanya.


Tunashukuru kwa ushirikiano wa viongozi wa kijiji, walimu, wazazi na wanafunzi chini ya Uratibu wa Afisa Maendeleo wa Kata ya Miono, Dada Bhoke Wambura. Tunaamini elimu hii itazaa matunda na kuendelea kujenga kizazi salama, kinachothamini utu na haki za kila mtoto.


Leave a Comment: