PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA SEMINA VIJIJI VYA MPERAUMBI NA KWALA

SEMINA MBALIMBALI Semina mbalimali

Posted by admin on 2025-08-21 15:21:20 | Last Updated by admin on 2025-09-19 10:53:47

Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 48


PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA SEMINA VIJIJI VYA MPERAUMBI NA KWALA

Ilikuwa ni semina ya siku moja kwa kila kijiji, Agosti 5 (Mperamumbi) na Agosti 6 Kwala. Walengwa wa Mafunzo:


Viongozi wa jamii wakiwemo viongozi wa serikali za Kata/vijiji/mitaa, viongozi wa dini, wazee wa mila, walimu, wahudumu wa afya, wahudumu ya jamii, wahudumu wa ustawi wa jamii, na viongozi wa vikundi vya wanawake na vijana.

Lengo Kuu la Mafunzo:

Kuwawezesha viongozi wa jamii kupata maarifa na stadi za kutumia mbinu shirikishi ili kutambua aina za ukatili wa kijinsia katika jamii yao na kupanga hatua za pamoja za kukabiliana na tatizo hilo.

Malengo Mahususi ya Mafunzo


Ifikapo mwisho wa mafunzo, washiriki wataweza:

1. Kufafanua maana ya GBV na kueleza aina, sababu, na athari zake.

2. Kutumia zana shirikishi ili kubaini GBV katika jamii.

3. Kuendesha mijadala salama na jumuishi kuhusu GBV.

4. Kushirikisha jamii katika kuandaa mikakati ya kukabiliana na GBV.


Leave a Comment: