Posted by admin on 2025-08-21 15:03:16 | Last Updated by admin on 2025-09-19 10:49:24
Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 47
Ukatili wa kijinsia ni janga linaloacha majeraha makubwa kwa mtu binafsi, familia, na jamii kwa ujumla. Kwa mtu mmoja mmoja, madhara yake yanaweza kuonekana kupitia msongo wa mawazo, huzuni, matatizo ya akili, maumivu ya mwili, ulemavu wa kudumu, magonjwa ya zinaa, mimba zisizotarajiwa, na kupoteza kujiamini. Wengi hujikuta wakijitenga na jamii na kushindwa kufikia ndoto zao.
Athari hizi huenea hadi kwenye familia, zikisababisha ndoa kuvunjika, migogoro ya kifamilia, na watoto kukosa malezi bora au kuiga tabia hatarishi. Katika jamii kwa ujumla, ukatili huongeza umaskini, unakwamisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na kuvuruga mshikamano na amani. Ni wajibu wetu wote kupaza sauti, kuelimisha, na kuchukua hatua kukomesha ukatili huu.