Posted by admin on 2025-10-25 14:29:39 |
Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 18
Mnamo tarehe 16 Oktoba 2025, wanafunzi
12 (wavulana 6 na wasichana 6) walihitimu mafunzo ya Safari
ya Uhuru wa Kifedha yaliyoandaliwa na Equip
for Change. Mafunzo haya yaliyofanyika Dar es Salaam, yalitumia
mwongozo wa African Money Map unaotokana na mafundisho ya Crown
Financial Ministries, unaosaidia watu kutembea katika safari ya
kiroho na kiuchumi kuelekea uhuru wa kifedha wa kweli.
Kupitia somo hili, washiriki walijifunza kanuni za Biblia
kuhusu:
l Umiliki
na usimamizi (stewardship) — kutambua kuwa Mungu ndiye mmiliki wa
yote; sisi ni wasimamizi wake.
l Kazi
kwa uaminifu na nidhamu — kufanya kazi kwa bidii na kwa moyo wote
kama kwa Bwana.
l Udhibiti
wa matumizi, kulipa madeni, kuokoa, na kutoa kwa ukarimu.
l Kujenga
uhusiano mzuri na Mungu, familia, na jamii kupitia uaminifu na uadilifu.
Washiriki walihimizwa kutekeleza walichojifunza nyumbani kwa
kuandaa bajeti, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, na kuanza kuweka akiba na kuiwekeza
kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Tunaamini kwamba haya ni mavuno mapya ya maisha yaliyobadilishwa
— safari ya kutoka katika utumwa wa madeni na matumizi mabaya ya fedha kwenda
kwenye uhuru wa kifedha unaomtukuza Mungu.
Mafunzo yaliendeshwa na Mkufunzi CFE, Rev. John Wambura